
“2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”
Zaburi 1:2-3
Nakumbuka mwaka 2024 nilikuwa na changamoto fulani ya kifedha. Na kwa namna moja au nyingine ile changamoto ilikuwa nje ya uwezo wangu kuitatua, hivyo nikaona ni lazima nitafute msaada zaidi kwa MUNGU kupitia neno lake na maombi. Na nilichofanya zaidi katika maombi haya ilikuwa ni kujikita zaidi katika kutafakari neno la MUNGU maana yeye amesema “…..Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. “na kwa sababu haya ni maelekezo aliyoyatoa yeye MUNGU mwenyewe kupitia neno lake, basi na mimi niliyapokea na kuyafanyia kazi, na chakuvutia nikuwa, ndani ya muda mdogo nilipata majibu yangu yote kama niliyokuwa ninahitaji na hivyo kuniwezesha kutatua changamoto zangu zote.
Binafsi ninamini kuwa kama kanuni hii ya kutafakari neno ilinisaidia mimi kupata matokeo basi na wewe pia ukitumia kanuni hii utapata matokeo hayo hayo pia.
Hebu jaribu kupata muda wa kusoma na KUTAFAKARI neno la MUNGU na utaona matokeo yake .
Barikiwa.
Ili kupata masomo zaidi, karibu kujiunga na group la Whatsapp https://chat.whatsapp.com/BIuZByb9xxJHWThgQtvzca
