
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”
Waebrania 11:6
Kama kuna jambo la muhimu sana kwetu kama Watoto wa Mungu basi litakuwa ni kuishi maisha yenye kumpendeza yeye (yaani Baba yetu wa Mbinguni). Na ndio maana yeye (Mungu) hutufundisha neno lakekila wakati, makusudi tujue ni nini haswa yeye anategemea sisi tufanye ambacho kitamfurahisha.
Lakini katika kutaka kupata muongozo zaidi kwa swala hili, basi andiko la utangulizi limeweka bayana kuwa kama tunataka kuishi maisha yenye kumpendeza Mungu basi ni lazima tuishi kwa Imani “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza…… Ebrania 11:6”
Na kama tulivyotangulia kusema katika masomo yaliyopita tunapoongelea, kuishi kwa Imani tumesema ni kuishi kwa kufuata muongozo wa neno la Mungu katika kila jambo, yaani kuishi kwa kufuata nini maandiko yanelezea katika kila maamuzi na kisha ndio maamuzi yafanyike.
Kwa hiyo shujaa wa Bwana hakikisha katika kila jambo unazingatia neno la Mungu linasemaje kuhusiana na hilo unalotaka kufanya na kisha fuata maelekezo yake, maana hayo ndio maisha ya Imani na yenye kumpendeza Mungu.








