Blog

  • KATIKA YEYE TUNA HAKI

    “na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.

    Matendo 13:39

    Moja wapo ya vitu muhimu tulivyovipokea baada ya kumwamini YESU kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu ni haki ya kuitwa mwana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo mimi na wewe kama Watoto wa Mungu tunayo haki ya kuwa na afya njema, msaada wa kiuchumi wakati wa nyakati ngumu na hata msaada wa hekima wakati tunapohitajika kufanya maamuzi sahihi katika mazingira magumu. Haki hizi zote zimepatikana kwa kule kumwamini Yesu kama mwokozi wako. Na lengo la hizo haki ni kukuwezesha wewe kuishi maisha ya furaha, mbali na kuonewa na shetani. Kwa hiyo ndugu mpendwa kama haufurahishwi na namna maisha yako yanavyoenenda basi simama katika zamu yako na kudai haki zako, maana ni katika maombi tu unaweza kupata kila kilicho chako, Barikiwa.

  • MCHUNGAJI MWEMA

    1.Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
    2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
    Zaburi 23:1-2

    Kazi ya mchungaji ni kulinda na kuwatunza kondoo wake. Na kazi ya YESU kama mchungaji wako ni kukulinda na kukupa hekima ya kufanya maamuzi sahihi Kila siku. Lakini ili yeye aweze kutekeleza huo MPANGO wake basi ni lazima wewe ukubali kumuamini na kufuata maelekezo yake. Zingatia sana kufuata maelekezo yanayotokana na Neno la MUNGU maana Kwa kufanya hivyo utamruhusu yeye kukuongoza Katika kutatua mahitaji Yako yote. Barikiwa.

  • NGUVU YA KUTAFAKARI NENO

    “2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
    3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”
    Zaburi 1:2-3

    Nakumbuka mwaka 2024 nilikuwa na changamoto fulani ya kifedha. Na kwa namna moja au nyingine ile changamoto ilikuwa nje ya uwezo wangu kuitatua, hivyo nikaona ni lazima nitafute msaada zaidi kwa MUNGU kupitia neno lake na maombi. Na nilichofanya zaidi katika maombi haya ilikuwa ni kujikita zaidi katika kutafakari neno la MUNGU maana yeye amesema “…..Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. “na kwa sababu haya ni maelekezo aliyoyatoa yeye MUNGU mwenyewe kupitia neno lake, basi na mimi niliyapokea na kuyafanyia kazi, na chakuvutia nikuwa, ndani ya muda mdogo nilipata majibu yangu yote kama niliyokuwa ninahitaji na hivyo kuniwezesha kutatua changamoto zangu zote.
    Binafsi ninamini kuwa kama kanuni hii ya kutafakari neno ilinisaidia mimi kupata matokeo basi na wewe pia ukitumia kanuni hii utapata matokeo hayo hayo pia.
    Hebu jaribu kupata muda wa kusoma na KUTAFAKARI neno la MUNGU na utaona matokeo yake .
    Barikiwa.

    Ili kupata masomo zaidi, karibu kujiunga na group la Whatsapp https://chat.whatsapp.com/BIuZByb9xxJHWThgQtvzca

  • SIRI YA KUTAFAKARI NENO


    “8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”
    Yoshua 1:8

    Ni ukweli usiopingika kuwa MUNGU anakuwazia mawazo mema na mazuri, mawazo ya kukustawisha na kukupa mafanikio tele. Na ndio maana huwa anakufundisha mara kwa mara kupitia neno lake ni nini ulio wajibu wako ili ufikie hayo mafanikio. Tambua kuwa MUNGU anataka ufanikiwe katika Biashara yako kwa kukuona unapata faidi mara dufu kwa kila juhudi unayoionesha katika kufanya kazi, tena MUNGU anapenda kukuona ukiwa unafanikiwa katika Afya yako kwa kuwa na uzima tele na hata uponyaji kila mara changamoto za ugonjwa zinapojitokeza na zaidi ya hayo MUNGU anapenda kukuona unafanikiwa katika maisha yako kwa ujumla.
    Lakini ili yeye aweze kufanya mambo hayo yote kuwa halisi kwako, MUNGU anayo mategemeo fulani kwako. Yeye anategema kuwa wewe utafanyia kazi maelekezo yake ya kutafakari neno kila siku ili kupitia njia hiyo aweze kukujaza na mawazo yenye kukuongoza katika kufikia mafanikio. Ndio maana katika andiko la utangulizi MUNGU anatuambia kuwa “ ….. bali yatafakari maneno yake mchana na usiku …….maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana”
    Kwa hiyo ndugu mpendwa hapo sasa wajibu ni kwako wa kufanyia kazi malekezo ya MUNGU na uone namna ambavyo atakufikisha katika kustawi sana. Barikiwa.

    Ili KUPATA masomo zaidi karibu kujiunga na group la Whatsapp https://chat.whatsapp.com/BIuZByb9xxJHWThgQtvzca

Design a site like this with WordPress.com
Get started